Katika kuendelea kuunga mkono maandamano ya amani yanayo endelea Iraq, na kuwakumbuka watu waliopata shahada kwenye maandamano pamoja na kuzipa pole familia zao na wapenzi wao, watumishi na wanafunzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atbatu Abbasiyya wanafanya maombolezo.
Uongozi wa chuo umesema kua: “Hakika chuo cha Al-Ameed kuanzia viongozi, wanavunzi na watumishi wake, kwa majonzi na masikitiko makubwa wanasoma dua ya kuwarehemu mashahidi walio uwawa kwenye maandamano katika mikoa tofauti ya Iraq, na kuwaombea majeruhi wapone haraka, sambamba na kulitakia amani na utulivu taifa letu kipenzi la Iraq”.
Msimamo wa chuo hiki ni sawa na misimamo ya taasisi zingine za kisekula hapa Iraq pamoja na wafanyakazi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wanaunga mkono maandamano ya amani ya kudai haki walizo pewa kikatiba na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu.
Chuo hakijaishia kufanya hivyo peke yake, bali siku za nyuma kilitangaza maombolezo na kusimamisha masomo kwa ajili ya kuwakumbuka mashahidi wa Iraq hasa walio uwawa kwenye maandamano ya amani huko Naswiriyya na Najafu, wanafunzi pia walishiriki katika maandamano na wakatoa huduma za kitabibu kwa waandamanaji.