Sauti ya raia: Haya ndio yaliyosemwa na Marjaa Dini mkuu mwezi (3 Rabiul-Awwal 1433h) sawa na (27 Januari 2012m).

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amekua akitahadharisha kwa miaka mingi hatari ya kuingiliwa siasa za ndani ya taifa la Iraq na watu wa nje, akavitaka vyama vya siasa kuwa kitu kimoja na kuzuwia kuingiliwa na watu wa nje, alitoa wito huo zaidi ya mara moja kupitia mimbari ya khutuba za Ijumaa.

Tunakuleteeni baadhi ya aliyosema kwenye khutuba ya Ijumaa ya mwezi (3 Rabiul-Awwal 1433h) sawa na (27 Januari 2012m) iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai katika haram ya Imamu Hussein (a.s), alisema kua: “Sababu ya msingi inayo fanya baadhi ya nchi jirani kuingilia siasa za Iraq ni kushambuliana kwa vyama vya siasa, jambo hilo limedhofisha taifa na kusabilia njia ya kuingiliwa na nchi jirani, aidha Iraq sio taifa imara kama mengine, pamoja na kuwa na vitu vingi vinavyo weza kulifanya kuwa taifa imara, ni taifa lenye utamaduni mzuri na linatakiwa kuwa kimbilio la majirani”.

Akaongeza kua: “Tunavitaka vyama vya siasa vilivyo chaguliwa na wananchi kuwa kitu kimoja, vinatakiwa viungane ili viweze kutekeleza wajibu wao ipasavyo, wananchi wanamatumani makubwa na wao, wanataka wapate amani na utulivu kisiasa na kiuchumi”.

Akabainisha kua: “Kila chama cha siasa kinatakiwa kijishushe kwa maslahi ya taifa na kutatua matatizo yaliyopo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: