Hospitali ya rufaa Alkafeel yapokea watu waliojeruhiwa kwenye maandamano ya Naswiriyya na yagharamia matibabu yao.

Maoni katika picha
Baada ya kutuma msafara wa kutoa misaada ya kimatibabu kwa watu waliojeruhiwa kwenye maandamano ya mkoani Dhiqaar, na baada ya kikosi cha madaktari kilicho tumwa huko na hospitali ya Alkafeel kuanza kazi kwa kushirikiana na hospitali ya Hussein (a.s), wamebaini majeruhi wanao hitaji matibabu zaidi au upasuwaji na wanao weza kusafirishwa hadi hospitali ya Alkafeel kupitia gari za wagonjwa, tayali wameanza kusafirishwa kwenda katika hospitali ya Alkafeel kuendelea na matibabu.

Fahamu kua jambo hili ni sehemu ya shughuli za kibinadamu zinazo fanywa na hosptitali ya Alkafeel, imekuwa ikiwatibu watu wanaojeruhiwa kwenye maandamano tangu siku ya kwanza ya maandamano hayo, chini ya program ya (matibabu bila malipo).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma kadhaa kwa waandamanaji, miongoni mwa huduma hizo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula kinacho pikwa katika mgawaha wa Atabatu Abbasiyya na kutumwa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa wakati tofauti.
  • - Kufanya usafi katika sehemu zinazo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia gari maalum za usafi.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji kwa waandamanaji.
  • - Kutoa huduma za matibabu bure kwa kila mtu anayepata matatizo ya afya kwenye maandamano raia au askari.
  • - Kujenga hema za kufundisha huduma ya kwanza na uwokozi kwa waandamanaji sambamba na kutoa huduma za uwokozi.
  • - Kutuma misafara ya kutoa misaada kwa waandamanaji katika uwanja wa uhuru mjini Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: