Kama kawaida Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba kamili ya kuomboleza msiba huu, ratiba hiyo inamambo yafuatayo:
- 1- Kupokea mawakibu za kuomboleza zitakazo ingia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuja kumpa pole kwa msiba huu mkubwa.
- 2- Kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram tukufu ya Abbasi kwa ajili ya mazuwaru.
- 3- Kufanya majlisi ya kuomboleza rasmi kwa ajili ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya ukumbi wa utawala.
- 4- Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) utagawa chakula kwa mazuwaru watakao omboleza msiba huu jirani na malalo ya Imamu Hussein na ngugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kumbuka kua wapenzi na wafusi wa Ahlulbait (a.s) kila kona ya dunia wanaomboleza kifo cha binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Fatuma Zaharaa (a.s), kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na mahala alipo zikwa (a.s), yote hii inaonyesha ukubwa wa dhulma aliyo fanyiwa, hadi akamuhusia kiongozi wa waumini Ali (a.s) afiche kaburi lake na wala jeneza lake lisishuhudiwe na yeyote miongoni mwa wale walio mdhulumu, alifariki akiwa na umri wa miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya mashuhuri.