Atabatu Abbasiyya tukufu yakanusha kujenga hema na vibanda vyake katika eneo la Babu Bagdad kaskazini ya mji wa Karbala.

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umekanusha kujenga hema na vibanda katika eneo la Babu Bagdad kaskazini ya mji wa Karbala, na imekubali kuwa inaunga mkono watu wanaofanya maandamano ya amani na inaendelea kutoa misaada katika uwanja wa Tarbiyya katikati ya mji wa Karbala.

Tamko hilo limetolewa baada ya kusambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kua; katika eneo hilo kuna hema la Atabatu Abbasiyya linapokea vijana kutoka mikoa mingine kwa ajili ya kufanya maandamano hadi Bagdad.

Ataba tukufu inaunga mkono maandamano ya amani kama yanavyo ruhusiwa na katiba ya Iraq na kupasishwa na Marjaa Dini mkuu, pia inasisitiza kushikamana na maelekezo ya Marjaa mkuu, ulazima wa kulinda amani kwa gharama yeyote, kama wanavyo fanya asilimia kubwa ya waandamanaji.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa misaada tofauti kwa waandamanaji wa Karbala, miongoni mwa misaada hiyo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula kinacho pikwa katika mgawaha wa Atabatu Abbasiyya na kutumwa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa wakati tofauti.
  • - Kufanya usafi sehemu zinazo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia kari maalum za usafi.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji kwa waandamanaji.
  • - Kutoa huduma za matibabu bure kwa kila mtu anayepata matatizo ya afya kwenye maandamano raia au askari.
  • - Kujenga hema za kufundisha huduma ya kwanza na uwokozi kwa waandamanaji sambamba na kutoa huduma za uwokozi.
  • - Kutuma misafara ya kutoa misaada kwa waandamanaji katika uwanja wa uhuru mjini Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: