Atabatu Abbasiyya tukufu yaweka wazi msimamo wake kuhusu maandamano ya kesho Ijumaa (6 Desemba).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa tamko kuhusu maandamano yatakayo fanyika kesho siku ya Ijumaa (6/12/2019m), imesema kua imealikwa kushiriki katika maandamano hayo kupitia waratibu wa maandamano ya kesho (6/12/2019m), kwa kua Ataba tukufu na watumishi wake ni sehemu ya jamii, imekubali kushiriki kwenye maandamano hayo.

Ataba imekua ikisaidia waandamanaji na bado inaendelea kuwasaidia katika mji wa Bagdad na mikoa kingine, kwa kuwapa chakula, maji na matibabu.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya inatoa misaada kadhaa kwa waandamanaji wa Karbala, miongoni mwa misaada hiyo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula kinacho pikwa katika mgawaha wa Atabatu Abbasiyya na kutumwa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa wakati tofauti.
  • - Kufanya usafi sehemu zinazo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia kari maalum za usafi.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji kwa waandamanaji.
  • - Kutoa huduma za matibabu bure kwa kila mtu anayepata matatizo ya afya kwenye maandamano raia au askari.
  • - Kujenga hema za kufundisha utowaji wa huduma ya kwanza na uwokozi kwa waandamanaji sambamba na kutoa huduma za uwokozi.
  • - Kutuma misafara ya kutoa misaada kwa waandamanaji katika uwanja wa uhuru mjini Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: