Ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mazuwaru wa kike wanaomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa majlisi ya wanawake kuomboleza kifo cha Swidiiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza, ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika sardabu ya Imamu Jawaad (a.s), wameshiriki mazuwaru na wakina mama wa kikundi cha Zainabiyyaat kwenye majlisi hiyo.

Katika majlisi hiyo imezungumzwa sehemu ya khutuba ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na kufafanua ukubwa wa fitina ya kuuchafua uislamu kuanzia zama zile hadi sasa, na namna bibi Zaharaa (a.s) alivyo pambana kuelekeza jamii.

Majlisi ikahitimishwa kwa tenzi za kuomboleza, na mwisho kabisa ikasomwa dua ya Imamu wa zama, na kuliombea amani na utulivu taifa la Iraq na wananchi wake pamoja na kuwarehemu mashahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: