Muhimu na hivi punde.. tamko la Marjaa Dini mkuu kuhusu matukio ya hivi karibuni katika maandamano.

Maoni katika picha
Limesomwa tamko la Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (9 Rabiul-thani 1441h) sawa na (6 Desemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s).

Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai amesema kua: mabwana na mabibi nakusomeeni nakala iliyotufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani mjini Najafu..

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Bila shaka harakati za wananchi zinapo husisha watu wa tabaka zote huwa ni njia kubwa ya kuwabana wenye mamlaka na kuwafanya watoe nafasi ya mabadiliko ya kweli katika taifa, lakini sharti la msingi ni kutosababisha uvunjifu wa amani, vurugu na uharibifu, pamoja na kutovunja sheria na kanuni, yasipo zingatiwa mambo hayo kutakua na matokeo mabaya yatakayo sababisha hasara, pamoja na kumwagika kwa damu tukufu katika kupigania kufikiwa malengo ya kisheria, lazima kuzinduka na kuchukua tahadhari kwa kuzuwia waovu wasiotaka islahi wasije wakajipenyeza na kuzuwia kupatikana kwa islahi.

Hakika kulinda usalama wa maandamano na kuhakikisha hayana uvunjifu wa amani wala uharibifu ni jambo muhimu sana, nalo ni jukumu la kila mtu, kama nilivyo sema jukumu hilo kimsingi ni la vyombo vya ulinzi na usalama, wao ndio wanajukumu la kuwalinda watu wanaofanya maandamano ya amani, na kuzuwia watu waovu wasijipenyeze kwa waandamanaji na kushambulia askari na mali za umma na raia na kusababisha matatizo kwa wananchi.

Hakika kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama na kuviheshimu pamoja na kuwapa moyo wa kutekeleza majukumu yao ya kulinda amani ni wajibu wa kila mtu, hatuwezi kuacha kuwategemea watu hawa muhimu katika kupambana na uvunjifu wa amani na vurugu, kila mtu ameona kilicho tokea katika baadhi ya miji, pale askari walipo shindwa kutekeleza majukumu yao, hadi viongozi wa makabila wakasimama imara kulinda amani na kuzuwia vurugu na uharibifu, yapasa kuwashukuru na kuwasifu kwa hilo, hakini hali inatakiwa irudi katika mazingira yake ya kawaida kwenye miji yote, jukumu la kulinda amani na usalama linatakiwa kuwa chini ya vyombo vya ulinzi na usalama, wao ndio wanawajibika kisheria kulinda usalama wa raia na mali zao, sambamba na kukagua kila kikundi cha waandamanaji yasije yakajirudia yaliyo tokea wiki zilizo pita.

Tunaendelea kulaani umwagaji wa damu na uharibifu wa mali za umma na raia ulio tokea siku za nyuma, tunatoa wito kwa waathirika weto wadai haki zao kwa kufuata sheria, tunaviomba vyombo vinavyo simamia utowaji wa haki vitoe adhabu kwa kila aliyefanya vitendo vya jinai kwa mujibu wa sharia.

Tunatoa onyo kwa wale wanaotaka kutumia maandamano ya wananchi kufikia malengo yao binafsi, tunarudia kusema yaliyo sisitizwa na Marjaa Dini mkuu yanawahusu wananchi wote wa Iraq bila kujali tofauti zao na milengo yao, analinda maslahi ya kila mtu kadri ya uwezo wake, haifai kutumiwa jina lake na kikundi chochote cha waandamanaji isije ikadhaniwa kuwa anaunga mkono kundi fulani tofauti na kundi lingine.

Mwisho ni matarajio yetu kua waziri mkuu mpya na baraza lake watachaguliwa ndani ya muda uliopangwa kikatiba kwa kuzingatiwa matakwa ya wananchi bila kuingiliwa na watu wa nje, ifahamike kua Marjaa Dini mkuu hana upande wowote katika swala hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: