Marjaa Dini mkuu: kulinda maandamano ya amani na kujiepusha na uvunjaji wa amani na uharibifu ni muhimu sana, pia ni jukumu la kila mtu.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu bado anaendelea kuhimiza maandamano ya amani, na kujiepusha na uvunjifu wa amani, swala ambalo ni muhimu sana, amesema kua jambo hilo ni jukumu la kila mtu, pia amesema kua vyombo vya ulinzi na usalama vinajukumu la kulinda watu wanaofanya maandamano ya amani, hali kadhalika waandamanaji wajizuwie kushambulia askari na kuharibu mali za umma na binafsi.

Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (9 Rabiul-Thani 1441h) sawa na (6 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), khutuba hiyo imesomwa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(kulinda maandamano ya amani na kujiepusha na uvunjifu wa amani na uharibifu ni muhimu sana, nalo ni jukumu la kila mtu, bila kusahau kuwa; wenye jukumu hilo ni vyombo vya ulinzi na usalama, vinatakiwa kuhakikisha usalama wa watu wanaofanya maandamano ya amani na kuwapa nafasi ya kusema matakwa yao kwa uhuru, pia ni jukumu la waandamanaji wenyewe kuzuwia waovu wasipipenyeze katika maandamano yao na kuwashambulia askari au kuharibu mali za umma na binafsi na kuharibu mustakbali wa raia).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: