Marjaa Dini mkuu: harakati ya raia inapo husisha watu wa tabaka zote ni njia ya kuwabana wenye mamlaka kutoa nafasi ya mabadiliko ya kweli.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesema kua harakati zinazo fanywa na wananchi wa Iraq za kudai haki zao kisheria, zitakapo husisha watu wa tabaka zote itakua ni njia ya kuwabana wenye mamlaka kufanya mabadiliko ya kweli bila kuchelewa, jambo kubwa harakati hiyo isijihusishe na uvunjifu wa amani, vurugu na uharibifu.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (9 Rabiul-Thani 1441h) sawa na (6 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), khutuba iliyosomwa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Bila shaka harakati za wananchi zinapo husisha watu wa tabaka zote huwa ni njia kubwa ya kuwabana wenye mamlaka na kuwafanya watoe nafasi ya mabadiliko ya kweli katika taifa, lakini sharti la msingi ni kutosababisha uvunjifu wa amani, vurugu na uharibifu, pamoja na kutovunja sheria na kanuni, yasipo zingatiwa mambo hayo kutakua na matokeo mabaya yatakayo sababisha hasara, pamoja na kumwagika kwa damu tukufu katika kupigania kufikiwa malengo ya kisheria, lazima kuzinduka na kuchukua tahadhari kwa kuzuwia waovu wasiotaka islahi wasije wakajipenyeza na kuzuwia kupatikana kwa islahi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: