Marjaa Dini mkuu anahimiza kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na kuvishajihisha kufanya majukumu yake ya kulinda amani na amepongeza viongozi wa makabila kwa kulinda watu wao na kuzuwia vurugu na uharibifu.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amehimiza umuhimu wa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kutekeleza wajibu wake wa kulinda amani, na amewashukuru viongozi wa makabila ya Iraq yaliyo linda watu wao na kuzuwia vurugu na uharibifu.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (9 Rabiul-Thani 1441h) sawa na (6 Desemba 2019m) katika haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Hakika kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama na kuviheshimu pamoja na kuwapa moyo wa kutekeleza majukumu yao ya kulinda amani ni wajibu wa kila mtu, hatuwezi kuacha kuwategemea watu hawa muhimu katika kupambana na uvunjifu wa amani na vurugu, kila mtu ameona kilicho tokea katika baadhi ya miji, pale askari walipo shindwa kutekeleza majukumu yao, hadi viongozi wa makabila wakasimama imara kulinda amani na kuzuwia vurugu na uharibifu, yapasa kuwashukuru na kuwasifu kwa hilo, hakini hali inatakiwa irudi katika mazingira yake ya kawaida kwenye miji yote, jukumu la kulinda amani na usalama linatakiwa kuwa chini ya vyombo vya ulinzi na usalama, wao ndio wanawajibika kisheria kulinda usalama wa raia na mali zao, sambamba na kukagua kila kikundi cha waandamanaji yasije yakajirudia yaliyo tokea wiki zilizo pita).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: