Marjaa Dini mkuu ametahadharisha kutumiwa jina lake na kundi lolote miongoni mwa makundi ya waandamanaji, isije ikadhaniwa kua anaunga mkono kundi fulani tofauti na kundi lingine, amesisitiza kua yeye anatetea raia wote wa Iraq bila kujali tofauti zao na milengo yao, ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa ya leo (9 Rabiul-Thani 1441h) sawa na (6 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) iliyo somwa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai.
Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Marjaa Dini mkuu anasisitiza kua yeye ni mtetezi wa wananchi wote wa Iraq bila kujali tofauti zao, anatetea maslahi ya kila mtu, wala haifai kundi lolote kutumia jina lake, isije ikadhaniwa kua anaunga mkono kundi fulani tofauti na kundi lingine).