Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimesema kua hakina uhusiano wowote na maandamano yanayo tarajiwa kufanyika tarehe kumi mwezi huu, yanayo itwa Rukdhwa Towareji (mapinduzi ya Hussein –a.s-).
Hayo yapo katika tamko maalum la kitengo hicho kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
(Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka) amesema kweli Mwenyezi Mungu mtukufu (surat A’raaf/158). Tangu Marjaa wetu mtukufu alipo kubali maandamano ya wananchi yanayo fanywa kila sehemu ya Iraq yetu madhulum, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hususan kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimekua na mchango mkubwa kwa waandamanaji, pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa watu wanaofanya maandamano ya amani tunatangaza kua, kitengo chetu hakina uhusiano wowote na maandamano yanayo andaliwa na watu wasio julikana yatakayo fanyika (10/12/2019m) yaliyo pewa jina la Rakdhwa Towareji (mapinduzi ya Hussein –a-s), yaliyo tangazwa kua yataanzia Karbala hadi Bagdad, baada ya kuwasiliana na viongozi wetu waliopo katika wilaya ya Hindiyya (Towareji) pamoja na baadhi ya washirika wetu na wawakilishi katika mikoa mingine, wamesema hawatambui maandamano hayo, kwa hiyo tunatoa taarifa rasmi kua hatuhusiki na maandamano hayo, Mwenyezi Mungu awanusuru raia wetu na taifa letu kipenzi kutokana na kila aina ya shari kwa utukufu wa Muhammad na watu wa nyumbani kwake watakasifu.