Katika uwanja wa Uhuru Karbala hadi kwenye uwanja kama huo Bagdad: watumishi wa Atabatu Abbasiyya wanadai islahi na kurudishwa haki za raia walizo nyangánywa.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshirikiana bega kwa bega na Ataba zingine pamoja na mazaru tukufu na wananchi wote wa Iraq kwenye maandamano makubwa, yaliyo pewa jina la (Maandamano ya Iraq ya pamoja) yaliyo fanywa jana mjini Bagdad, baada ya kualikwa na waratibu wa maandamano hayo ukizingatia kua Ataba tukufu ni sehemu ya jamii ya wananchi wa Iraq.

Maandamano hayo yaliyo fika hadi katika uwanja wa Tahriir (Uhuru) jijini Bagdad yamefanywa na watu kutoka mikoa tofauti ya Iraq, wakitanguliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na Ataba zingine na mazaru tukufu, wamesisitiza ulazima wa kutekelezwa madai ya wananchi ya kufanya marekebisho kwenye sekta ya wanasiasa na kuondoa ufisadi, kwa ajili ya kupatia maisha bora kila raia wa taifa hili.

Miongoni mwa mambo waliyodai waandamanaji ni kupitisha kanuni za uchaguzi huru na wa haki, kanuni zitakazo mfanya kiongozi awajibike kwa watu walio mchagua na awatumikie, kanuni zitakazo zuwia ununuzi wa madaraka na kura.

Tambua kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilituma msafara wa gari kwenye uwanja wa Tahriir (Uhuru) mjini Bagdad kushiriki kwenye maandamano hayo.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya hutoa misaada mbalimbali kwa waandamanaji, miongoni mwa misaada hiyo ni:

  • - Kuandaa maelfu ya sahani za chakula kinacho pikwa katika mgawaha wa Atabatu Abbasiyya na kutumwa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa wakati tofauti.
  • - Kufanya usafi sehemu zinazo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia gari maalum za usafi.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji kwa waandamanaji.
  • - Kutoa huduma za matibabu bure kwa kila mtu anayepata matatizo ya afya kwenye maandamano raia au askari.
  • - Kujenga hema za kufundisha utowaji wa huduma ya kwanza na uwokozi kwa waandamanaji sambamba na kutoa huduma za uwokozi.
  • - Kutuma misafara ya kutoa misaada kwa waandamanaji katika uwanja wa uhuru mjini Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: