Kwa kumfanyia upasuwaji: kikosi cha madaktari wa hospitali ya Alkafeel chaokoa maisha ya muandamanaji.

Maoni katika picha
Kwa kumfanyia upasuwaji mkubwa uliochukua saa tano, kikosi cha madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanikiwa kuokoa maisha ya muandamanaji aliyekua na tatizo kichwani, majeruhi wa hivi karibuni katika maandamano ya Karbala.

Daktari bingwa wa upasuwaji kutoka Uturuki Mustafa Aghakoni ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Jopo la madaktari chini ya uongozi wetu limefanikiwa kufanya upasuwaji wa jicho la kijana mwenye umri wa miaka (17) kutoka Karbala”, akasema: “kijana huyo alijeruhiwa wakati wa maandamano, na hospitali ya Alkafeel imemfanyia upasuwaji bure, upasuwaji huo umefanywa na madaktari bingwa wa macho wa Iraq na Uturuki”.

Aghakoni amesema kua: “Upasuwaji umechukua zaidi ya saa tano na umefanikiwa kutokana na umahiri wa madaktari pamoja na kuwepo vifaa tiba vya kisasa, akasisitiza kua afya ya kijana inaendelea kuimarika na ataruhusiwa baada ya siku chache”.

Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel, mwanzoni wa mwezi wa Desemba (2019) ilitangaza kua; imesha toa huduma ya matibabu kwa waandamanaji (1584) asilimia kuwa walikua na majeraha makubwa na walihitaji uwangalizi maalum, sambamba na kutoa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi wa kwenye maandamano ya mkoa wa Dhiqaar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: