Chini ya kauli mbiu isemayo: (Maktaba za wanawake ni mshirika mkubwa katika kufanikisha maendeleo endelevu kupitia utamaduni), ofisi ya wanawake chini ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya inaendelea na mradi wake wa (mafuriko ya utambuzi) unao lenga kujenga na kukarabati maktaba za serikali na binafsi, kwa ajili ya kutunza maarifa na kuyasambaza kwa njia rahisi na wakati muwafaka.
Hivi karibuni wamekamilisha ukarabati wa maktaba tatu, ambazo ni: maktaba ya shule ya Faidhu Zaharaa, shule binafsi ya Dini, shule ya sekondari ya wasichana Nabaa Adhim ambyo ni ya serikali, matkaba yake ipo kwenye majengo ya Abbasi ya makazi, pamoja na maktaba zingine zilizo tangulia, hii ni kutokana na maelezo ya kiongozi wa idara ya wanawake bibi Asma Ibadi, akaongeza kua: “Tumeunda kikosi kazi cha watalamu wa maktaba kwa ajili ya kuangalia mahitaji ya maktaba na kuandaa mkakati wa kutatua mahitaji hayo”.
Akabainisha kua: “Kazi ilianza miezi tisa iliyo pita, kwa kufanya vikao na kuingia makubaliano ya kiofisi na kiutendaji, baada ya kupokea maombi kutoka kwenye maktaba hizo, sasa hivi tunakaribia kumaliza matengenezo ya maktaba tatu na kuzikabidhi kwenye taasisi zake”.
Kuhusu ukamilifu wa kazi zingine kwa mujibu wa maelezo ya Abadi: “Tumefanya upembuzi wa vitabu vyenye majina yanayo fanana na vyenye mada zisizo faa, halafu tumetengeneza utambulisho maalum na kubaini kurasa kwa kutumia faharasi ya mada, pamoja na kuandika kwenye orodha inayo itwa (Sijilli Thabtu), halafu vitabu vimewekwa kwa mpangilio mzuri unao pendeza kuangalia, baada ya kumaliza kubandika karatasi za utambulisho juu yake”.
Akaendelea kusema: “Pamoja na kazi hizi tunasambaza machapisho ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile vitabu, majarida, pamoja na machapisho ya idara ya watoto”.
Akasisitiza kua: “Kufanya kazi na taasisi yeyote kunafungua milango zaidi ya harakati za kitamaduni, na hilo ndio lengo la harakati za maktaba”.