Ushiriki mkubwa wa mawakibu za kutoa huduma katika uwanja wa uhuru kuwaunga mkono waandamanaji.

Maoni katika picha
Tangu yalipo anza maandamano hapa Iraq, mawakibu za kutoa huduma zinazo fungamana na idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya zimekua mstari wa mbele kusaidia waandamanaji.

Mawakibu hizo pia zimekuwa na mchango mkubwa kwa waandamanaji walioweka kambi katika uwanja wa uhuru (tahriir) mjini Bagdad, mchango wao umeonekana wazi katika maandamano yaliyo fanyika hivi karibuni, ambampo wamefanya mambo yafuatayo:

 • - Kushirikiana na waratibu wa maandamano.
 • - Kutuma shehena za chakula na vitu vingine.
 • - Kujenga mabanda kwa ajili ya kutoa huduma kwa waandamanaji katika uwanja wa uhuru.
 • - Kushiriki katika maandamano.

Idara za Karkha na Raswafa zinamchango mkubwa kwazi zipo kila siku, kumbuka idara ya ustawi wa jamii tangu yalipo anza maandamano haya, imesimama pamoja na waandamanaji katika uwanja wa uhuru mjini Bagdad, na kwenye mikoa mingine, wanatoa huduma tofauti, kama vile:

 • - Kujenga mabanda ya kutolea huduma.
 • - Kuandaa chakula na kukigawa kwa waandamanaji.
 • - Kugawa chakula, maji na juisi kwa waandamanaji.
 • - Kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi.
 • - Kutoa huduma ya kwanza ya kitabibu na uwokozi.
 • - Wajumbe wengi wa mawakibu kuwepo katika uwanja wa maandamano.
 • - Kugawa baadhi ya vifaa vinavyo tumiwa na waandamanaji.
 • - Kusaidia kazi za kujitolea kama vile kufanya usafi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: