Chuo cha Al-Ameed na Zaharaa vinajadili kuhusu nyanja za elimu ya sekula.

Maoni katika picha
Ugeni kutoka chuo kikuu cha Zaharaa (a.s) chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu ukiongozwa na Dokta Zainabu Abdulhussein Sultani pamoja na jopo la wakufunzi wa chuo, wametembezea chuo cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kufungua milango ya ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja.

Ugeni huo umepokelewa na rais wa chuo Dokta Mu-ayyad Imraan Ghazali, wamejadili mambo mengi kuhusu sekta za elimu, na ushirikiano katika mambo ya kielimu baina ya vyuo hivyo.

Dokta Sultani amefurahishwa na maendeleo ya chuo kikuu cha Al-Ameed na akaomba kuwepo ushirikiano wa kielimu baina ya vyuo hivyo, wafanye makongamano, nadwa, warsha pamoja na tafiti mbalimbali kwa kushirikiana, sambamba na kubadilishana uzowefu kati yao, kwa namna ambayo kutakua na matokeo chanya katika taifa letu kipenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: