Sauti ya raia: haya ndio yaliyo semwa na Marjaa Dini mkuu mwezi (17 Rabiul-Awwal 1433h) sawa na (10/02/2012m).

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza mara nyingi kuhusu umuhimu wa kufanyiwa ukaguzi taasisi za serikali na wizara zake, kwa ajili ya kuhakikisha taasisi hizo zinawajibika ipasavyo na kuleta maendeleo kwa taifa.

Tunakuleteeni vipengele muhimu alivyo ongea kwenye khutuba ya Ijumaa ya mwezi (17 Rabiul-Awwal 1433h) sawa na (10/ 02/ 2012m), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), alisema kua: Uangalizi upo wa aina mbili: wa mtu anaye amini akhera, anakua anaamini kua Mwenyezi Mungu ndio mkaguzi wake, na mtu wa kawaida ambaye anahitaji kusimamiwa na sharia pamoja na kanuni”.

Sayyid Swafi akafafanua kua: “Mtu anapo hisi kua atakaguliwa hua na aina fulani ya umakini kazini”.

Akasema: “Kama hakuna ukaguzi baadae tatizo lazima litaonekana, hakika ukaguzi unafaida nyingi, yapasa kukagua matumizi ya pesa, ili zisitumike kwa mambo mengine tofauti na yaliyo pangwa”.

Akahoji kua: “Taasisi za ukaguzi zinafanya nini?! Naamini zipo nyingi, wingi wake unafaida gani?!! Simaanishi kua hakuna haja ya kua na taasisi za ukaguzi, lakini lazima tupate mrejesho wa kazi zao, tuelewe kama zimefikia malengo yao”.

Akasema: “Baadhi ya taasisi za ukaguzi katika nchi zingine huwa zinateua watu maalum wa kufanya kazi hiyo”.

Akaongeza kua: “Watu hao hupewa mamlaka ya kushtaki pale utakapo gundulika ubadhirifu katika taasisi za serikali, jambo hilo husababisha watumishi wa serikali kuwa makini kwa sababu wanaogopa kushtakiwa, hujitahidi kufuata kanuni ili wasitiwe hatiani”.

Akafafanua kua: “Lengo la kuwepo ukaguzi ni kuzuwia ufisadi, hivi tumesha pewa taarifa ya ukaguzi ya kweli?” Akahoji: hivi miradi ya serikali inakaguliwa? Kwa nini mtumishi ahisi kua wakaguzi ni maadui zake na sio watu salama kwake? Kwa nini watumishi hawafundishwi matumizi sahihi ya ofisi?.

Akaongeza kua: “Yapasa kutoa motisha kwa watumishi bora na tutumie uzowefu wa mataifa mengine, yanayo toa tuzo kwa watumishi bora”.

Akasisitiza kua: “Lazima kuwe na uwiyano baina ya pesa iliyo tumika sehemu stahiki na ile iliyotumika mahala pasipo stahiki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: