Wanafunzi wa maahadi ya Quráni tawi la wanawake wamepata ushindi mkubwa katika masomo ya tajwidi.

Maoni katika picha
Wanafunzi wa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdad chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamepata nafasi za juu katika mradi wa (Taratiilu Zaharaa) kwenye usomaji wa kufuata misingi muhimu ya tajwidi, semina inayo simamiwa na idara ya ufundishaji wa Quráni chini ya idara ya tabligh ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeshiriki idadi kubwa ya wanafunzi ambapo wamesoma tajwidi kwa mujibu wa riwaya ya Hafswa iliyo pokewa na Aaswim Kufiy pamoja na sherehe sambamba na kuhifadhi matini ya Jazriyya.

Mwanfunzi Ruqayyah Audah amepata alama (98.5) kwenye maswali ya kielimu na alama (99) kwenye maswali ya usomaji, naye Haafidhat Zaharaa Audah amepata alama (98) kwenye maswali ya kielimu na alama (97) kwenye maswali ya usomaji.

Hii sio mara ya kwanza wanafunzi wa Quráni katika Maahadi tawi la wanawake kupata ufaulu wa aina hiyo, mashindano yote waliyo shiriki siku za nyuma walipata alama za juu, hii ni ishara kua Maahadi inautaratibu mzuri kwenye ufundishaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: