Tamko la kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika kumbukumbu ya ushindi wa Iraq.

Maoni katika picha
Katika kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu upatikane ushindi wa Iraq, ulio letwa na raia wa Iraq dhidi ya magaidi wa Daesh, kwenye vita ambayo kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Liwaau/ 26 Hashdi Shaábi kilikua na nafasi kubwa katika kupatikana ushindi huo, kimetoa tamko kuhusu swala hilo, ifuatayo ni nakala la tamko hilo:

Kumbukumbu ya ushindi wa Iraq, tukio muhimu katika nafsi zetu, siku ya kuikomboa Mosul mji ambao ulionyesha ramani ya kupatikana kwa amani na utulivu wa Iraq, baada ya kuushinda utawala wa kikhalifa wa Daesh, adui ambaye alifanya kila aina za jinai.

Wananchi wa Iraq walipigana vita kubwa na magaidi wa Daesh, walimwaga damu takatifu kwa ajili ya kulinda taifa na utukufu wao, wakapata ushindi baada ya ushindi, kwa utukufu wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Sistani kutokana na fatwa yake tukufu, iliyo itikiwa na wapiganaji watukufu na kila aliyesimama pamoja nao kwa namna moja au nyingine, na wakaendelea kusimama pamoja hadi baada ya ushindi, wakaonyesha ubinadamu na uzalendo wa hali ya juu, wakaweza kuvunja njama kubwa ya mji mkuu wa ugaidi, sambamba na kujitolea kusiko kua na kifani na damu nyingi iliyo mwagika.

Tunatumia nafasi hii kutangaza msimamo wetu dhidi ya taifa na raia watukufu, sisi ni wazalendo tupo tayali kujitolea kila kitu kwa ajili ya taifa letu na raia wake, kama tulivyokua wa kwanza kuingia katika uwanja wa vita na kutoa mashahidi wengi, tunasisitiza kuendelea kufanya hivyo madam kutakuwa bado kuna haki tunayo nyimwa.

Kabla ya kumaliza yatupasa kuwarehemu mashahidi watukufu ambao damu zao zilimwagika kwa sababu ya kuitikia wito wa fatwa tukufu na wakafia taifa lao, tunawaombea dua ya kupona haraka majeruhi wote, aidha Mwenyezi Mungu ampe msimamo na uwezo kila atakaye fuata mwenendo wao, tunamuomba Mwenyezi Mungu alipe amani na utulivu taifa letu kipenzi la Iraq.

Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji

Liwaau/26 Hashdi Shaábi

9 Desemba 2019m.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: