Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya yahitimisha semina ya fani za adhana na misingi yake.

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za kueneza utamaduni wa Quráni hapa nchini, Maahadi ya Quráni tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha semina ya fani za adhana na misingi yake iliyo dumu kwa muda wa siku nne, ambapo wamefundishwa sauti na naghma sambamba na misingi ya kusoma adhana na namna zake, mkufunzi wa semina hiyo alikua ni Ustadh Twalibu Ifaari na ilikua na washiriki zaidi ya 40.

Hafla ya kufunga semina imefunguliwa na kiongozi wa tawi Sayyid Haamid Marábiy, amewapongeza washiriki na amesifu juhudi zao, akaeleza lengo la semina hiyo ambalo ni kulinda misingi ya fani hii isiharibiwe na baadhi ya wasomaji wa adhana.

Mwishoni wa hafla hiyo wanasemina wakapewa vyeti vya ushiriki, nao wameishukuru Atabatu Abbasiyya pamoja na wasimamizi wa semina hii kwa juhudi kubwa waliyo nayo ya kutumikia vizito viwili vitakatifu.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya hufanya semina mbalimbali zinazo husu usomaji wa Quráni katika kipindi cha mwaka mzima na kwenye mikoa tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: