Katika kuenzi damu zao takatifu na kufanyia wema familia zao: kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinakaribia kukamilisha nyumba ya mmoja wa mashahidi.

Maoni katika picha
Katika kuenzi kazi nzuri iliyofanywa na familia za mashahidi kwa namna walivyo jitolea watoto, ndugu na wazazi wao, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kinagawa nyumba kwa familia za mashahidi watukufu, kikosi kinakaribia kukamilisha nyumba ya mmoja na mashahidi wake aitwae Shahidi Mahadi Ahmadi Jaluut.

Shekh Maitham Zaidi kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji amesema kua: Ujenzi umefanywa kwa ufadhili wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi chini ya muda maalum na kwa viwango vinavyo endana na utukufu wa shahidi huyo.

Akasisitiza kua: “Tunatarajia kufanya uzinduzi wa nyumba hiyo baada ya wiki mbili”.

Akasema: “Kadri tunavyo jitahidi kutoa kwa ajili ya mashahidi bado tunajiona sawa na hatujafanya kitu”.

Tambua kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kwa kusaidiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na utendaji wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, kinatekeleza mradi wa (Nyumba za makazi Alwafaa) ambazo zinajengwa rasmi kwa ajili ya makazi ya familia za mashahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: