Katika kusaidia na watu wanao jeruhiwa kwenye maandamano: chuo kikuu cha Al-Ameed na hospitali ya Alkafeel zafanya zowezi la kujitolea dadu.

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa kujitolea kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa waandamanaji, chini ya utaratibu iliyo jipangia, chuo kikuu cha Al-Ameed na hospitali ya rufaa Alkafeel zimeandaa zowezi la kujitolea damu, kwa ajili ya kusaidia watu walio jeruhiwa kwenye maandamano ya Karbala na mikoa mingine.

Zowezi hili limebeba ujumbe mwingi, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono madai ya waandamanaji.

Makumi ya wafanyakazi wa chuo kikuu wakiongozwa na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na makamo kiongozi wa idara Dokta Alaa Mussawi na idadi kubwa ya viongozi wa vitengo pamoja na wanafunzi, wamejitokeza kujitolea damu kama sehemu ya kusaidia majeruhi.

Kwa mujibu wa waliojitokeza kujitolea damu, zowezi hilo linalenga kusaidia hazina kuu ya damu ya mkoa, kwani damu ni kitu muhimu sana kinacho hitajiwa na majeruhi, hususan wakati huu ambao taifa linashuhudia maandamano makubwa ya kudai mabadiliko katika serikali na maisha bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: