Muhimu na hivi punde.. tamko la Marjaa Dini mkuu kuhusu hali inayo endelea hivi sasa Iraq.

Maoni katika picha
Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ambaye ni muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo mwezi (16 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (13 Desemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), amesoma tamko kutoka ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu.

Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema kua: Mabwana na mabibi nakusomeeni nakala iliyotufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Hussein Sistani katika mji wa Najafu..

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Siku chache zilizo pita tumeadhimisha mwaka wa pili tangu litolewe tangazo la kuwashinda magaidi wa Daesh, tukio kubwa la kihistoria la vita kali waliyo pigana wananchi wa Iraq kwa ajili ya kukomboa miji iliyokua imetekwa na magaidi wa Daesh, katika vita hiyo iliyo chukua zaidi ya miaka mitatu makumi ya maelfu ya mashahidi walipatikana pamoja na idadi kubwa ya majeruhi, ikaandikwa historia ya utukufu na ushujaa wa Iraq katika kulinda ardhi, heshima na maeneo matakatifu.

Tukio hilo tukufu ndani ya nyoyo za wairaq wote tunawakumbuka kwa heshima kubwa mashahidi watukufu walio lowesha udongo wa taifa hili kwa damu zao takatifu, wakapata daraja kubwa la utukufu, tunawakumbuka kwa heshima kubwa wao na familia zao pamoja na watu wote waliojeruhiwa na waliopata ulemavu, nawale ambao bado wanaendelea kuugulia maumivu ya mabaki ya magaidi, na wanaendeleza mapambono nao kwa ushujaa mkubwa katika maeneo tofauti, tunawashukuru sana na kuwaombea dua kwa ikhlasi.

Yatupasa kusisitiza yale tuliyosema kuhusu umuhimu wa jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vya Iraq vinapaswa kua chini ya misingi madhubuti, vinapaswa kulinda taifa dhidi ya uwadui wowote kutoka nje sambamba na kulinda utaratibu wa kisiasa unaotokana na matashi ya wananchi chini ya katiba, tunaendelea kusisitiza ulazima wa kuboresha maisha katika miji iliyo kombolewa, na kuijenga upya ili kuwawezesha wakazi wa miji hiyo waliopo katika kambi za wakimbizi warejee kwenye miji yao kwa heshima na amani.

Enyi wairaq watukufu.. hakika mpo katika vita kubwa (vita ya islahi) na kuutokomeza ufisadi uliodumu kwa kipindi kirefu, pamoja na uzembe katika idara za serikali, Marjaa Dini mkuu alisisitiza katika khutuba ya ushindi miaka miwili iliyo pita kua: (Hakika vita hii –iliyo chelewa sana- haina tofauti na vita dhidi ya ugaidi au hii ni ngumu zaidi, raia wa Iraq walioshinda vita dhidi ya ugaidi –kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu- wanaweza kupigana vita hii na kushinda kama wakijipanga vizuri katika idara zao), hakika kutumia njia za amani ndio sharti kubwa la kushinda vita hii, jambo muhimu ni kwamba asilimia kubwa ya waandamanaji wanatambua ulazima wa kufanya maandamano ya amani na kujiepusha na vitendo vya ukatili na vurugu sambamba na kulinda mali za wananchi, pamoja na damu zote zilizo mwagika kwa dhulma na uonevu, tukio la mwisho la umwagaji wa damu ni lile lililotokea mwanzoni mwa wiki hii la kushambuliwa waandamanaji katika eneo la Nasaki mjini Bagdad, tukio ambalo makumi ya watu wamekufa na wengine kujeruhiwa.

Hakika tukio hilo linaumiza, aidha matukio ya utekaji yaliyo fanyika siku za nyuma yanathibitisha umuhimu wa madai ya Marjaiyya, ulazima wa kuweka siraha zote chini ya serikali na kutoruhusu kikundi chochote kumiliki siraha kwa jina lolote, hakika utulivu wa taifa na kulinda amani kunategemea swala hilo, tunatarajia iwe hivyo mwasho wa vita ya islahi.

Tunalaani mauwaji na utekaji uliotokea, likiwemo tukio baya lililotokea jana katika mji wa Wathaba, tunatoa wito kwa wahusika kuwafichua waliofanya jinai hiyo na kuwaadhibu kwa mujibu wa sharia, tunaomba jambo hilo lisitokee tena, kwani linaharibu maandamano ya amani yanayo takiwa kulindwa na kila mtu, aidha tunasisitiza ulazima wa kuwa na mahakama huru, kwani ndio kimbilio pekee kwa kila jinai na makosa yanayo fanywa, isuruhusu kutoa adhabu hata kwa anayestahiki ispokua kwa kufuata njia za kisheria na kanuni za adhabu, uuwaji, kusulubu maiti, kufunga watu juu (kuningíniza) mambo hayo pia ni jinai, hayatakiwi kufanywa, jambo la kuhuzunisha sana ni yaliyo shuhudiwa kwa kukusanyika watu wengi kuangalia ukatili uliofanyika jana, hakuna hila wala nguvu ispokua kwa Mwenyezi Mungu mkuu na mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: