Marjaa Dini mkuu amezungumzia kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu kutolewa kwa tangazo la ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, akasema kua ilikua vita kali na mtihani mkubwa kwa wananchi wa Iraq, vita hiyo imeacha maelfu ya mashahidi na majeruhi, wameandika historia ya ushujaa na utukufu, amewataja kwa heshima na taadhima mashahidi walio mwaga damu zao takatifu katika ardhi ya taifa lao, wakapata daraja kubwa na utukufu, akazipongeza familia zao tukufu pamoja na majeruhi na watu waliopata ulemavu, pamoja na wale ambao bado wanaendelea kupigaba hadi sasa kulinda taifa lao.
Ameyasema hayo katika khutuba ya leo (16 Rabiul-Aakhar) sawa na (13 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) iliyo somwa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Siku chache zilizo pita tumeadhimisha mwaka wa pili tangu litolewe tangazo la kuwashinda magaidi wa Daesh, tukio kubwa la kihistoria la vita kali waliyo pigana wananchi wa Iraq kwa ajili ya kukomboa miji iliyokua imetekwa na magaidi wa Daesh, katika vita hiyo iliyo chukua zaidi ya miaka mitatu makumi ya maelfu ya mashahidi walipatikana pamoja na idadi kubwa ya majeruhi, ikaandikwa historia ya utukufu na ushujaa wa Iraq katika kulinda ardhi, heshima na maeneo matakatifu.
Tukio hilo tukufu ndani ya nyoyo za wairaq wote tunawakumbuka kwa heshima kubwa mashahidi watukufu walio lowesha udongo wa taifa hili kwa damu zao takatifu, wakapata daraja kubwa la utukufu, tunawakumbuka kwa heshima kubwa wao na familia zao pamoja na watu wote waliojeruhiwa na waliopata ulemavu, na wale ambao bado wanaendelea kuugulia maumivu ya mabaki ya magaidi, na wanaendeleza mapambono nao kwa ushujaa mkubwa katika maeneo tofauti, tunawashukuru sana na kuwaombea dua kwa ikhlasi).