Marjaa Dini mkuu amerudia kusisitiza umuhimu wa jeshi na vikosi vya wapiganaji kuwa chini ya serikali kuu.
Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (16 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (13 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo somwa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Yatupasa kusisitiza yale tuliyosema kuhusu umuhimu wa jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vya Iraq vinapaswa kua chini ya misingi madhubuti -serikali kuu-, vinapaswa kulinda taifa dhidi ya uadui wowote kutoka nje sambamba na kulinda utaratibu wa kisiasa unaotokana na matashi ya wananchi chini ya katiba).