Tangu kutangazwa ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh na kurudisha miji iliyokua imetekwa na magaidi hao, Marjaa Dini mkuu ameongea katika zaidi ya khutuba moja kuhusu umuhimu wa kujenga maeneo yaliyo kombolewa, na kusaidia kurudi watu waliokimbia miji yao kutokana na vita.
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa leo (16 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (13 Desemba 2019m) iliyotolewa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.
Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Tunaendelea kusisitiza ulazima wa kuboresha maisha katika miji iliyo kombolewa, na kuijenga upya ili kuwawezesha wakazi wa miji hiyo waliopo katika kambi za wakimbizi warejee kwenye miji yao kwa heshima na amani).