Marjaa Dini mkuu amesisitiza mara nyingi kua utulivu wa Iraq unategemea siraha zoto kuwa chini ya serikali kuu, na kuto ruhusu kikundi chochote cha wapiganaji kumiliki siraha kwa kisingizio chochote, akasema kua matukio ya mauaji na utekaji yaliyo tokea hivi karibuni yanatokana na tatizo hilo.
Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo lililo tolewa kwenye khutuba ya Ijumaa leo (16 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (13 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi:
(Hakika tukio hilo linaumiza, aidha matukio ya utekaji yaliyo fanyika siku za nyuma yanathibitisha umuhimu wa madai ya Marjaiyya, ulazima wa kuweka siraha zote chini ya serikali na kutoruhusu kikundi chochote kumiliki siraha kwa jina lolote, hakika utulivu wa taifa na kulinda amani kunategemea swala hilo, tunatarajia iwe hivyo mwasho wa vita ya islahi).