Marjaa Dini mkuu amelaani mauaji na utekaji aidha ametahadharisha vitendo hivyo visijirudie.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amelaani mauaji na utekaji vilivyo tokea jana katika mji wa Wathaba, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini wahalifu hao na wengine pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (16 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (13 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Tunalaani mauwaji na utekaji uliotokea, likiwemo tukio baya lililotokea jana katika mji wa Wathaba, tunatoa wito kwa wahusika kuwafichua waliofanya jinai hiyo na kuwaadhibu kwa mujibu wa sharia, tunaomba jambo hilo lisitokee tena, kwani linaharibu maandamano ya amani yanayo takiwa kulindwa na kila mtu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: