Marjaa Dini mkuu amesisitiza ulazima wa kua na mahakama huru kwani ndio kimbilio kwa kila aina ya jinai zinazo fanywa.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza ulazima wa kua na mahakama huru kwani ndio kimbilio kwa aina zote za jinai zinazo fanywa, aidha ametahadharisha utowaji wa adhabu bila kufuata sharia.

Amehuzunishwa na yaliyo tokea hivi karibuni katika mji wa Wathaba, mauaji, utekaji na udhalilishaji wa maiti, akasema kua wahalifu waliofanya mambo hayo inabidi wahukumiwe.

Lifuatalo ni tamko lililo tolewa kuhusu swala hilo katika khutuba ya leo (16 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (13 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi:

(Aidha tunasisitiza ulazima wa kuwa na mahakama huru, kwani ndio kimbilio pekee kwa kila jinai na makosa yanayo fanywa, isuruhusu kutoa adhabu hata kwa anayestahiki ispokua kwa kufuata njia za kisheria na kanuni za adhabu, uuwaji, kusulubu maiti, kufunga watu juu (kuningíniza) mambo hayo pia ni jinai, hayatakiwi kufanywa, jambo la kuhuzunisha sana ni yaliyo shuhudiwa kwa kukusanyika watu wengi kuangalia ukatili uliofanyika jana, hakuna hila wala nguvu ispokua kwa Mwenyezi Mungu mkuu na mtukufu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: