Marja Dini mkuu: asilimia kubwa ya waandamanaji wanajua umuhimu wa kuandamana kwa amani na kujiepusha na uhalifu jambo hilo linatia moyo.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kufanya maandamano ya amani, akasema kua hilo ndio sharti kubwa la ushindi, asilimia kubwa ya waandamanaji wanatambua hilo.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa ya leo (16 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (13 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Hakika kutumia njia za amani ndio sharti kubwa la kushinda vita hii, jambo muhimu ni kwamba asilimia kubwa ya waandamanaji wanatambua ulazima wa kufanya maandamano ya amani na kujiepusha na vitendo vya ukatili na vurugu sambamba na kulinda mali za wananchi, pamoja na damu zote zilizo mwagika kwa dhulma na uonevu, tukio la mwisho la umwagaji wa damu ni lile lililotokea mwanzoni mwa wiki hii la kushambuliwa waandamanaji katika eneo la Nasaki mjini Bagdad, tukio ambalo makumi ya watu wamekufa na wengine wengi kujeruhiwa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: