Ukarimu wa wairaq katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) wajadiliwa katika mkutano wa turathi na utamaduni (UNESCO)

Maoni katika picha
Shirika la elimu na utamaduni la umoja wa mataifa (UNESCO), limejadili huduma wanazo pewa watu wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) katika upeo wa kimataifa, kwenye mkutano wa kumi na nne uliofanyika mji mkuu wa Kolombia Boghota, na kuhudhuriwa na zaidi ya wajumbe (900) kutoka nchi (153).

Muwakilisho wa Iraq kwenye mkutano huo alikua ni kiongozi wa mashirika ya kimataifa katika sekta ya uhusiano wa kitamaduni kwenye wizara ya utamaduni na utalii Imani Abdulwahaab, amesema kua: “Taarifa iliyo wasilishwa na kituo cha Karbala cha masomo na utafiti katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imepasishwa na kupigiwa kura na nchi wanachama zilizo shiriki katika mkutano huo”.

Naye Ustadh Amiri Kaamil muwakilishi wa kituo cha Karbala cha masomo na tafiti ambaye ni miongoni mwa wajumbe wa Iraq walioshiriki kwenye mkutano huo amesema kua: “Mkutano wa kumi na nne uliofanywa Boghota mji mkuu wa Kolombia, kuanzia tarehe (8 – 14 Desemba), umeamua kuingiza vikundi vinavyo toa huduma katika ziara ya Arubaini kwenye orodha ya turathi zisizo kua za kawaida kwa binadamu, imepigwa kura ya pamoja na kuunga mkono hoja bila pingamizi lolote”.

Fahamu kua taarifa hiyo iliandaliwa na kituo cha Karbala cha masomo na tafiti, imewasilishwa kwa jina la Jamhuri ya Iraq kupitia wizara ya utamaduni, chini ya itifaki maalum za kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: