Maahadi ya Quráni tukufu na kitengo cha tabligh katika ofisi ya Ayatullah mtukufu Sayyid Muhammad Saidi Hakim wanajadili kuhusu kufanya kazi kwa pamoja na kufungua milango wa ushirikiano.

Maoni katika picha
Ugeni wa kitengo cha tabligh kutoka ofisi ya Mheshimiwa Ayatullah mtukufu Sayyid Muhammad Saidi Hakim pamoja na Maahadi ya Quráni tawi la Najafu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamejadili kuhusu kufungua milango ya ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja katika kueneza utamaduni unaoendana na mafundisho ya Quráni tukufu.

Hayo yamejiri katika ziara iliyofanywa na ugeni ulio ongozwa na Shekh Muhammad Abadi kiongozi wa idara ya mipango na harakati katika kitengo cha tabligh, na Shekh Muayyad Abadi kiongozi wa idara ya mawasiliano na tabligh ya nje ya kitengo, katika ofisi ya tawi huko Naafu, walipokelewa na kiongozi wa tawi hilo Sayyid Muhandi Majidi Haamid Almayahi.

Wakajadili kuhusu ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja kati ya Maahadi na kitengo cha tabligh, katika mambo yanayo husiana na miradi ya Quráni inayo endeshwa na wanafunzi wa Dini, na kuongeza juhudi ya kueneza elimu na maarifa ya Quráni.

Kiongozi wa tawi la Maahadi ya Quráni ameeleza kuhusu harakati zinazo fanywa na Maahadi tangu ilipo anzishwa hadi mwisho wa mwaka huu, miongoni mwa shughuli za kijamii na semina za Quráni, pamoja na nadwa za Quráni kwa watu wenye umri tofauti, akafafanua harakati zinazo fanywa na Maahadi kwa wanafunzi wa Dini.

Wageni wamepongeza kazi zinazo fanywa na Maahadi, wakawatakia mafanikio mema katika kazi hiyo tukufu inayo ridhiwa na kupendwa na muumba wetu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: