Kupitia ofisi zake katika mkoa wa Baabil: Idara ya ustawi wa jamii inaendelea kusaidia waandamanaji kwenye mikoa mitatu.

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ofisi zake za mikoani pamoja na mawakibu zinazo fungamana nayo, inaendelea kusaidia watu wanaofanya maandamano ya amani, ikiwa ni pamoja na ofisi ya Baabil ambayo inafanya kila iwezalo kusaidia waandamanaji kwenye mikoa mitatu (Baabil, Karbala na Bagdad).

Kwa mujibu wa wasimamizi wa zowezi hilo, utowaji wa misaada umegawanyika sehemu tatu: kwanza ni kutuma misafara ya misaada kwenye viwanja vya waandamanaji (uwanja wa Tahriri) Bagdad, ambako wamepewa vitu mbalimbali vinavyo wasaidia kuendelea kupaza sauti kuhusu madai yao.

Sehemu ya pili ni misaada inayotolewa kwa waandamanaji wa Baabil, kupitia mabanda ya kutoa misaada, ambapo hugawa chakula na kutoa misaada ya matibabu na mingineyo.

Sehemu ya tatu ni kwenye mkoa wa Karbala katika uwanja wa Ahraar ambako wanagawa chakula kwa waandamanaji.

Fahamu kua idara ya ustawi wa jamii tangu yalipo anza maandamano haya imekua mstari wa mbele kusaidia waandamanaji kuanzia uwanja wa Tahriri mjini Bagdad, na wameenea katika viwanja vya waandamanaji kwenye mikoa mingine, miongoni mwa huduma wanazo toa ni:

  • - Kujenga mabanda ya kutolea misaada.
  • - Kugawa chakula kwa waandamanaji.
  • - Kugawa maji na juisi.
  • - Kutoa huduma za uokozi na matibabu.
  • - Kusaidia kuokoa majeruhi kwa kutumia gari za wagonjwa.
  • - Ushiriki wa watumishi wa mawakibu katika viwanja vya maandamano.
  • - Kugawa baadhi ya vifaa vinavyo tumiwa na waandamanaji.
  • - Kusaidia kufanya usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: