Katika kuwaendeleza kielimu na kitabligh: Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya yaratibu warsha kwa watumishi wake.

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa semina za kuwajengea uwezo wahadhiri wa Husseiniyya, idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha warsha ya namna ya kupambana na mashambulizi ya kifikra na kubadilisha fikra hasi kuwa chanya, kwa wahadhiri wa mimbari ya Husseiniyya, chini ya usimamizi wa wataalam kutoka wabebaji wa ujumbe wa Zainabiyya.

Bibi Taghridi Tamimi kiongozi msaidizi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Warsha hii ni sehemu ya mkakati wa kuwajengea uwezo wahadhiri wa mimbari ya Husseiniyya na kuwafanya waendane na mazingira tunayo ishi, katika warsha hii tumejikita katika mambo muhimu ya namna ya kuamiliana na fikra hasi zisizo za kweli na namna ya kupambana nazo kielimu kwa hoja na dalili”.

Akasema kua: “Warsha imejumuwisha wahadhiri kutoka maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Karbala pamoja na kuonyesha nafasi ya Atabatu Abbasiyya katika swala hilo”.

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa idara hii ni kusaidia kuimarisha tablighi katika sekta ya wanawake, kutokana na umuhimu wao hasa wakati wa kipindi cha maombolezo, na kuwatoa pembezoni, kwa kuwafanya waweze kuelezea tukio la Imamu Hussein kielimu na kwa njia inayo fahamika vizuri na inayo endana na mazingira halisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: