Kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Al-Ameed kimeshiriki katika kongamano la kimataifa kuhusu saratani, kongamano hilo limeandaliwa na umoja wa madaktari katika chuo kikuu cha Qatar kwa kushirikiana na jumuiya ya saratani ya Qatar, pamoja na jumuiya ya mashariki ya kati ya tafiti za maradhi ya saratani (MEACR), washiriki wa kongamano hilo ni viongozi, madaktari na taasisi mbalimbali.
Chuo cha Al-ameed kimewakilishwa na Dokta Samiir Hassan Rikabi na makamo mkuu wa chuo Dokta Rahim Mahadi, kongamano limejadili njia za matibabu ya saratani na namna ya kuboresha ushirikiano wa taasisi zinazo fanya kazi kwenye sekta hiyo kitaifa na kimataifa.
Ushiriki wa kitivo cha udaktari umewasilisha chapisho linalozungumzia maradhi ya saratani ya damu na namna ya kuyatibu, chapisho ambalo washiriki wote wamelisifu kutokana na maelezo yaliyomo kwenye chapisho hilo, pamoja na mada za kitafiti zilizo wasilishwa na mijadala mbalimbali iliyo fanywa katika kubadilishana mawazo na uzowefu.
Kumbuka kua kongamano hili huandaliwa kila mwaka na jumuiya ya mashariki ya kati ya tafiti za saratani, shirika lisilokua la biashara lililo amzishwa kwa lengo la kukusanya wataalam wa saratani, watafiti na wadau wa maradhi ya saratani pamoja na wanafunzi wa elimu ya juu, lengo la kongamano hili ni kupeana taarifa na kubadilishana uzowefu kati ya vyuo tofauti na taasisi za elimu katika mashariki ya kati.