Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya watembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Alkafeel.

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea watu waliojeruhiwa kwenye maandamano ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel, majeruhi hao wametoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, madaktari na wauguzi wanafanya kila wawezale katika kuwapa huduma.

Ujumbe huo umehusisha (kitengo cha Dini, kitengo cha uhusiano na kitengo cha habari na utamaduni), wameangalia hali za majeruhi na wakawaombea wapone haraka, aidha ujumbe huo uliwafikishia salamu za watumishi wa Atabatu Abbasiyya pamoja na dua zao kwao, wakagawa zawadi za kutabaruku na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na zawadi zingine.

Ujumbe umesifu kazi nzuri inayo fanywa na watumishi wa hospitali ya rufaa Alkafeel na wakawaomba waendelee na juhudi hizo.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya inatoa misaada mbalimbali kwa waandamanaji, miongoni mwa misaada hiyo ni:

  • - Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya hupika chakula na kwenda kukigawa kwa waandamanaji kwa kutumia gari.
  • - Hufanya maandamano pamoja na waandamanaji wengine na kutoa misaada ya kibinadamu katika uwanja wa maandamano mjini Karbala.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa nyakati tofauti.
  • - Kufanya usafi kwa kutumia gari maalum za usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji ya kunywa kwa waandamanaji.
  • - Kutoa huduma za matibabu kwa watu waliopata matatizo ya afya kwenye maandamano raia au askari.
  • - Kufunga vipaza sauti katika uwanja wa maandamano mjini Karbala.
  • - Kujenga hema za kutoa mafunzo ya uokozi na huduma ya kwanza kwa waandamanaji.
  • - Kutuma misafara ya kutoa misaada kwa waandamanaji katika uwanja wa Tahriir mjini Bagdad.
  • - Kusaidia kusafirisha waandamanaji kutoka Karbala hadi Bagdad katika siku za maandamano makubwa.
  • - Kusaidia kutoa huduma ya matibabu kwa watu walio jeruhiwa kwenye maandamano ya mkoani Diqaar.
  • - Kufanya majlisi za kuomboleza watu waliouwawa kwenye maandamano ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: