Khutuba za Ijumaa zinazo tolewa Karbala huandikwa na nani?

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbsiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ameongea kuhusu uandishi wa khutuba ya pili ya Swala ya Ijumaa inayo tolewa katika haram ya Imamu Hussein (a.s), ambayo mara nyingi huongelea mazingira halisi wanayo ishi raia wa Iraq.

Sayyid Swafi ameongea katika mahojiano na luninga yaliyo naswa na mtandao wa kimataifa Alkafeel, amesema kua: “Hakika hutuba ya pili katika swala ya Ijumaa hupatikana kwa moja ya njia mbili, kuna wakati huandikwa nakala rasmi kwa mkono wa Mheshimiwa Sayyid Sistani kutokana na umuhimu wa jambo, na wakati mwingine huashiria nukta muhimu za kuongelea”.

Akabainisha kua: “Hakika khutuba ya pili lazima tupate idhini kutoka kwa Mheshimiwa, au yeye mwenyewe hutuambia cha kuongea”, akasema kua: “Hakika fatwa ya jihadi kifaya ilikua ni nakala iliyo andikwa na Mheshimiwa Sayyid Sistani, hali kadhalika khutuba ya ushindi iliyo fungamana na matukio ya Kurdistan pamoja na mambo ya maelekezo ya kiidara, khutuba hizo zipo katika mtandao wa Mheshimiwa Sayyid Sistani”.

Fahamu kua mara nyingi khutuba ya pili katika swala ya Ijumaa inayo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) huongelea mambo ya kisiasa na maelekezo ya kijamii, na hutolewa kwa zamu baina ya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na Mheshimiwa Shekh Mahdi Karbalai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: