Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chatangaza kukamilisha utaratibu wa kusajili wanachama wake.

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kimetangaza kua kimemaliza jukumu lake la kuwarudisha kazini wanachama wake, kikasema kua kinasubiri msimamo wa kamati ya Hashdi Shaábi pamoja na wizara ya fedha kuhusu swala hilo.

Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) ulichukua hatua zifuatazo katika kutekeleza jukumu hilo:

  • - Kikosi kilikamilisha vielelezo vyote muhimu kuhusu swala hilo, kiliandaa fomu maalum na kuwasilishwa kwenye kamati ya Hashdi Shaábi.
  • - Kikosi kiliandaa kamati maalum katika mwezi wa Novemba kwa ajili ya swala hilo, iliyo kua na jukumu la kupokea wanachama kwenye vituo vya kikosi cha Abbasi, wale walio jitolea kushiriki katika kutekeleza majukumu ya kikosi wakiwemo wapiganaji wa Hashdi Shaábi walio shiriki katika matukio manne kwa uchache, na wale ambao majina yao yapo katika orodha maalum ya kikosi hata kama hayata onekana kwenye kumbukumbu ya kamati ya Hashdi Shaábi, ukitoa wapiganaji walio simamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu na makosa ya kivita.

Kikosi kimesisitiza kua: “Hatujapata igizo jipya lolote kwa ajili ya utekelezaji, jambo hili linahitaji maelekezo ya kamati iliyo undwa chini ya kifungu cha (107) cha mwaka huu kilicho undwa na baraza la mawaziri, kinacho zungumzia kuwarudisha kazini wanachama wote wa vikosi vya wapiganaji na kuwaweka chini ya wizara ya ulinzi na Hashdi Shaábi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: