Upasuaji wa aina yake: kuondoa uvimbe wa kwenye mgongo wa mtoto mwenye umri wa miaka sita katika hospitali ya rufaa Alkafeel.

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel mjini Karbala chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa upasuwaji wa mtoto mwenye umri wa miaka sita, aliyekua anasumbuliwa na uvimbe wenye uzito wa kilo mbili (kg 2) kwenye mgongo, uliokua umeenea kwenye uti wa mgongo hadi katika mishipa ya moyo.

Tumeongea na Dokta Mustafa Aghukoni kuhusu upasuaji huo, amesema kua: “Jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kumtibu mtoto mwenye umri wa miaka sita, aliye kua anasumbuliwa na uvimbe wa mgongoni ulio sambaa hadi kwenye mishipa ya moyo”.

Naye Dokta Bashiri Akbanazi bingwa wa upasuaji kutoka uturuki akasema kua: “Hakika uvimbe ulikua umeenea sehemu ya mgongoni hadi kwenye mishipa ya moyo”. Akasema kua: “Jopo la madaktari bingwa wa upasuwaji limefanikiwa kuondoa uvimbe huo pamoja na kusafisa eneo lote na kuondoa chembechembe zote za uvimbe”.

Akafafanua kua kua: “Baada ya saa 24 za upasuaji hali ya afya ya mtoto iliimarika, huku akiwa chini ya uangalizi wa jopo la madaktari bingwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: