Maahadi ya watoto yenye uwezo wa kujifunza Alkafeel chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, imechukua jukumu la kutoa mafunzo chini ya ratiba maalum, kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa mambo mbalimbali kimasomo na kimaadili.
Aidha Maahadi inasaidia kuongeza uwezo wa masomo na kufanya kazi kwa wanafunzi, kwa namna ambayo itawasaidia kuishi na jamii bila kikwazo chochote.
Yote hayo yanafanyika chini ya selebasi maalum inayo tumiwa na Maahadi ya watoto wenye mahitaji maalum Alkafeel.
Kumbuka kua Maahadi inapokea watoto wenye ulemavu (wanao weza kujifunza), aina za walemavu wanao chukuliwa ni wale wenye mtindio wa ubongo, au wenye mazingira ya ukimywa na wenye matatizo ya kinafsi pamoja na watoto wenye matatizo ya kutamka sambamba na wale wenye tatizo la upweke usio pitiliza.