Marjaa Dini mkuu mwaka 2012: Iwapo bunge halitajali mahitaji ya wananchi jambo hilo litawavunja moyo raia na kuleta matatizo siku za mbele.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu alitahadharisha mara nyingi wana siasa wasifanye mambo yatakayo wavunja moyo raia wa Iraq, kwani jambo hilo ni hatari katika siku zijazo, kama wasipo fanya mabadiliko ya kweli katika kushughulikia matatizo ya wananchi.

Tunakumbusha baadhi ya yaliyo semwa katika khutuba ya Ijumaa ya mwezi (8 Rabiul-Thani 1433h) sawa na (2 Machi 2012m), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai katika ukumbi wa hayam ya Imamu Hussein (a.s), alizungumzia swala la kupigiwa kura kwa mswada ya kutengwa dinari (bilioni 60) kwa ajili ya kununua (gari 350) za wabunge, Shekh Karbalai akafafanua kua: michango ya baadhi ya wabunge wanaopinga maoni ya Marjaa na wananchi (yaliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu pamoja na raia kwa ujumla) haikubaliki, wala hiendani na watu walio chaguliwa kuwakilisha raia wa Iraq, wala hatutaki kuingia katika swala hilo kwa undani.

Shekhe Karbalai akalitaka bunge libadilishe matumizi ya pesa hizo na kuzielekeza katika mambo mengine ya miradi ya kuhudumia wananchi, au zisaidie kutibu majeruhi au kusaidia mayatima na wajane.

Karbalai akasema kua hatua hiyo itawafanya wananchi wahisi kua bunge limebadilika na sasa limeanza kushugulikia matatizo ya raia, limekua bunge sikivu linalo fanyia kazi matatizo ya wananchi, wabunge pia wataonekana wanajali na kuumizwa na matatizo ya raia na kutanguliza maslahi ya wananchi na wala sio maslahi yao binafsi.

Mheshimiwa Shekh Karbalai akatahadharisha kufanya kinyume na hivyo, kama bunge halitajali matakwa ya wananchi jambo hilo litaleta matatizo siku za mbele na wananchi watakosa Imani na wabunge wao, pia wananchi watavunjwa moyo na wanasiasa, na hilo ni jambo hatari kwa mustakbali wa taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: