Msafara wa (Alwafaa lidimaau shuhada) unao ratibiwa na idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya, umekwenda kutembelea familia za watu waliopata shahada kwenye maandamano, kituo chake cha kwanza ni familia za mashahidi wa mkoa wa Dhiqaar kwenda kuwapa pole kwa kupotelewa na wapenzi wao.
Kiongozi wa idara tajwa hapo juu Shekh Abbasi Akaishi amesema kua: “Tumewasili Dhiqaar mji wa ukarimu, kujitolea na mashahidi, tukiwa na mawakibu za watu wa Bagdad, Karkha na Diyala, tumetembelea familia za mashahidi na kuwapa misaada sambamba na kuwapa pole kutokana na kuwapoteza wapenzi wao”.
Akaongeza kua: “Msafara huu utatembelea familia zote za mashahidi katika mikoa ya Iraq”.
Familia za mashahidi zimesema kua mji wa Dhiqaar ni miongoni mwa miji yenye matatizo makubwa na uliojeruhiwa kwa kupoteza wapezi wao walio pata shahada kwenye maandamano yanayo ungwa mkono na Marjaa Dini mkuu kwa kuwa ni maandamano ya kudai haki za raia kisheria.
Wakabainisha kua: “Mashahidi walikua katika tabaka la vijana baadhi yao walikua ni wahitimu wa vyuo, walitoka kuandamana kwa ajili ya kudai maisha bora katika mji wa Dhiqaar na Iraq kwa ujumla pamoja na kudai ajira ikiwa ni sehemu ndogo sana ya haki zao”.
Familia za mashahidi zimetoa shukrani za dhati kwa msafara huu uliokuja kuwaliwaza na kuwapa pole.