Marjaa Dini mkuu na msimamo wake kuhusu maandamano mwaka (2011): mambo aliyotaka na kutahadharisha wakati huo.

Maoni katika picha
Kupambana na ufisadi ni swala lililopo katika sekta tofauti za serikali, na kuchukua maamuzi magum ya kuacha marupurupu yasiyo kubalika, wanayo pewa wabunge wa sasa na wa zamani kwenye vikao vya bunge na mikoa, pamoja na viongozi wakuu serikalini kama vile mawaziri na wenye mamlaka maalum, na kuondoa vyeo visivyo kua na umuhimu serikalini, ambavyo vinaligharimu taifa pesa nyingi sana za raia wanyonge, akatahadharisha kuendelea na utaratibu wa sasa katika idara za serikali.

Haya ni mambo muhimu aliyo tahadharisha Marjaa Dini mkuu wanasiasa, yapo katika tamko lililo tolewa mwaka (2011) kufuatia maandamano ya wananchi –wakati huo- yaliyo kua yanadai mabadiliko, uhuru na maisha bora.

Lifuatalo ni tamko lililotolewa (22 Rabiul-Awwal 1432h) sawa na (26 Februari 2011m):

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Hakika Marjaa Dini mkuu anapinga kushambuliwa wa wananchi watukufu walio shiriki kwenye maandamano ya amani yaliyo fanywa jana, na anatoa wito kwa bunge na serikali ya Iraq zichukue hatua madhubuti, katika kuboresha huduma za jamii hususa umeme na vitu vingine, na kutoa ajira sambamba na kupambana na ufisadi ulioenea katika idara tofauti za serikali, kabla ya kila kitu inatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kuondoa marupurupu yasiyo kubalikwa wanayo pewa wabunge wa sasa na wa zamani pamoja na ofisi za mikoa na viongozi wa juu serikalini mawaziri na wengine, aidha kuondoa vyeo visivyokua vya lazima serikalini ambavyo vinaligharimu taifa pesa nyingi sana za raia wanyonge kila mwaka.

Hakika Marjaa Dini mkuu amekua akisisitiza sana umuhimu wa kufanyia kazi madai ya wananchi, na kutahadharisha kuendelea kwa utaratibu wa sasa katika idara za serikali, na kinacho weza kutokea kama hayatotatuliwa matatizo ya wananchi waliyo yavumilia kwa muda mrefu.

(Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuongoze sote katika mambo yenye kheri hakika yeye ni mwingi wa kusikia na mwingi wa kujibu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: