Marjaa Dini mkuu ameonyesha kusikitishwa na hali ngumu inayo pitia taifa kutokana na kuendelea kwa maandamano ya amani, akasema kua kuna watu wengi wanao lalamikia udhaifu wa dola na baadhi ya watu kujiona wako juu ya sheria na kufanya kila kitu bila hofu wala kizuwizi.
Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (23 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (20 Desemba 2019m) katika haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai.
Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo: (Bado taifa linaishi katika mazingira magumu, bado kuna makundi ya watu yanaendelea kushiriki kwenye maandamano ya amani ya kudai islahi, huku watu wengine wakitekwa na kupewa vitisho, na upande mwingine ofisi nyingi za serikali na taasisi za elimu zinalazimishwa kufunga milango bila kuwepo na ulazima wa kufanya hivyo, huku mali za baadhi ya raia zikichomwa na kuharibiwa, watu wengi wanalalamikia udhaifu wa vyombo vya dola na baadhi ya watu kujiona wako juu ya sheria kwa hiyo wanafanya jambo lolote bila uoga).