Marjaa Dini mkuu: Wananchi ndio msingi wa utawala na uhalali wa serikali unategemea wao, njia rahisi na salama ya kututoa kwenye matatizo tuliyo nayo ni kurudi kwa raia.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kufanya uchaguzi wa mapema baada ya kuunda kanuni na sheria za uchaguzi, akasema kua jambo hilo ndio njia rahisi na salama ya kututoa kwenye matatizo ya taifa kwa sasa, yanayo taka kulidumbukiza taifa kwenye vurugu na vita ya ndani, ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (23 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (20 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Katika khutuba ya kwanza tumesema kua wananchi ndio msingi wa utawala na uhalali wa serikali unategemea wao –kama ilivyo kwenye katiba-, kwa hiyo njia salama ya kututoa kwenye matatizo tuliyo nayo na yanayo weza kusababisha vita ya ndani –Allah atuepushie- ni kurudi kwa wananchi, kwa kufanya uchaguzi wa mapema na kuweka sheria na kanuni zitakazo wezesha kuwa na uchaguzi huru na wa haki, sambamba na kuwa na wasimamizi huru katika ngazi zote ili kurudisha uaminifu wa uchaguzi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: