Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kupasisha haraka kanuni za uchaguzi na ziendane na matakwa ya raia.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kupasisha kanuni za uchaguzi na zinatakiwa ziendane na matakwa ya raia wa Iraq, kanuni zitakazo wawezesha kuchagua viongozi wanao wataka watakao saidia kulitoa taifa katika matatizo.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (23 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (20 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai.

Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Lakini tunaona ucheleweshwaji wa kutunga kanuni za uchaguzi hadi leo, bado wabunge wanatofautiana katika mambo ya msingi, tunasisitiza tena umuhimu wa kufanya haraka kupitisha kanuni za uchaguzi tena ziendane na madai ya wananchi, zitakazo wawezesha kufanya uchaguzi huru na wa haki, kanuni hizo zinatakiwa zitukwamue katika matatizo tuliyo nayo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: