Marjaa Dini mkuu anaonyesha nafasi ya wasomi wazalendo wenye uwezo kuingia katika siasa baada ya kupitishwa kanuni za uchaguzi zinazo kubalika.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ameonyesha umuhimu wa kuingia katika siasa wasomi wazalendo wenye uwezo baada ya kupasishwa kanuni za uchaguzi zinazo kubalika, aidha amesema kua kampeni zinatakiwa kua za ushindani wa elimu na uwezo wa kutatua matatizo ya taifa, sio za kikabila, kikanda na kimadhehebu, kila mtu achaguliwe kutokana na uwezo alionao na sio vinginevyo.

Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (23 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (20 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai.

Lifuatalo ni tamko kuhu swala hilo:

(Kazi ya kuandaa kanuni ikikamilika itafuata hatua ya kuchagua wanasisa wazalendo, na kupanga safu ya watu madhubuti watakao weza kuleta maendeleo ya taifa na kumaliza matatizo tuliyo nayo, kisha zifanyike kampeni za ustaarabu wala sio za kutukanana au ubaguzi wa kivyama, miji, koo au madhehebu, bali wagombea wajinadi kwa sifa zao kielimu na kiweledi sambamba na mikakati watakayo kuja nayo ya kuliondoa taifa katika matatizo tuliyo nayo na kulifikisha mahala bora, tunatarajia bunge lijalo na serikali yake ifanye marekebisho muhimu ya kulitoa taifa kwenye makucha ya ufisadi, upendeleo na kukosekana kwa uadilifu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: