Atabatu Abbasiyya tukufu inaadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya Dhwadi.

Maoni katika picha
Kituo cha masomo na utafiti cha kimataifa Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Ijumaa (23 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (20/12/2019m) kimefanya hafla ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya kiarabu na kuhudhuriwa na wasomi wengi wa sekula.

Hafla hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa kituo cha Al-Ameed na kufunguliwa kwa Quráni tukufu halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukafuata ujumbe wa kituo ulio wasilishwa na Dokta Aadil Nadhiir, akaanza kwa kuwarehemu mashahidi wa Iraq, wanajeshi wa serikali na hashdi Shaábi pamoja na mashahidi wa vita ya islahi, akasema kua: “Hakika lugha ya kiarabu inahaki ya kuadhimishwa, bado ipo katika misingi yake chini ya watafiti, ni lugha yenye maneno mengi sana, inamaneno zaidi ya milioni kumi na mbili”.

Akaongeza kua: “Lugha ya kiarabu inahaki ya kuadhimishwa kutokana na mchango wake kwa binadamu na uwepo wake, ni lugha ambayo imewapa wanadamu urithi mkubwa usiokua na mfano, hakuna lugha yeyote iliyompa mwanadamu urithi mkubwa zaidi ya kiarabu, kiarabu ni lugha pekee yenye vitabu vingi zaidi duniani, maktaba ya kiarabu ni moja ya maktaba kubwa za lugha duniani”.

Akaendelea kusema kua: “Quráni tukufu ina nafasi kubwa ya kulinda na kuitunza lugha ya kiarabu, Atabatu Abbasiyya imekua mstari wa mbele katika kuanzisha na kufanya miradi inayo tunza lugha ya kiarabu, kwa kuchapisha majarida maalum ya masomo ya lugha ya kiarabu pamoja na kufanya makongamano na nadwa”.

Halafu ukafuata ujumbe wa kamati ya kulinda lugha ya kiarabu kutoka baraza la mawaziri, ulio wasilishwa na rais wa kamati hiyo Dokta Karim Hussein Alkhaalidiy, akasema kua: “Lugha ya kiarabu imepambana na kila aina ya upotoshwaji, imeendelea kua kinara wa elimu, maarifa, semi na ufasaha”. Akasema: “Mtume wetu (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) wana heshima kubwa kwa kuanzisha masomo ya kiarabu kama vile Nahau, Swarafu, Balagha na fani mbalimbali za lugha”.

Kisha ukaingia muda wa mashairi ya kiarabu fasaha, akapanda kwenye mimbari mshairi Dokta Alawi Kaadhim na Ustadh Sajjaad Abdulhamiid, waliosoma shairi linalo onyesha kuipenda lugha ya dhwadi.

Baada yao ukafuata waraka wa utafiti ulio wasilishwa na Dokta Muhammad Hussein Ali uliokua na anuani isemayo: (Maudhui ya kidigitali katika lugha ya kiarabu baina ya uhalisia na utendaji).

Hafla ikahitimishwa kwa kugawa vyeti vya ushiriki kwa watoa mada, washairi na waandishi wa habari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: